Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

(TCRA-CCC)

Zingatia!!

  • Usiongee na simu au kutuma au kupokea ujumbe mfupi wakati unaendesha gari au chombo chochote cha moto na unapovuka barabara.
  • Usiongee na simu inapokuwa iko katika umeme
  • Usifanye uhalifu wa kutumia kifaa cha Mawasaliano au huduma kwa kuwa ni kinyume cha sheria.
  • Ukipoteza simu yako au laini ya simu toa taarifa polisi na kwa mtoa huduma wako.
  • Ukiokota simu au laini (kadi) ya simu usivitumie.Toa taarifa polisi inawezekana vitu hivyo vinahusishwa na uhalifu na unaweza kuingia matatani.
  • Usimpe mtu yoyote laini (kadi) yako ya simu bila kutoa taarifa kwa mtao huduma wako na kubadili usajili.
  • Jisajili unaponunua laini ya simu kinyume cha hapo utakua unavunja sheria na adhabu yake ni kubwa.
  • Kama ni mfanyabiashara ya kuuunganisha watumiaji kwa kuwapatia laini, usitoe laini kwa mtu yeyote bila kuandikisha maelezo yake na kuona kitambulisho chake halisi; vinginevyo utakuwa unavunja sheria.
  • Usitoe namba zako za siri unazotumia kwenye huduma mbalimbali kupitia simu yako ili kuepuka kuibiwa au kutapeliwa.