Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano
Kifungu cha 93(1) cha Sheria hii kinaainisha kwamba kila mwenye simu au anayetarajiwa kununua simu ya mkononi anawajibika kisheria kusajili namba yake. Kifungu hicho hicho cha 93(2) kinafafanua kila anayeuza sim card anawajibika kusajili namba ya simu kabla haijaanza kutumika.
Mabadiliko yoyote ya taarifa katika usajili wa sim-card yafanyike kwa mtoa huduma katika kipindi cha siku 15 tangu kutokea kwa mabadiliko hayo(96).
Usajili wa namba za simu za mikononi una madhumuni ya kumlinda mtumiaji na vitendo visivyofaa vinavyofanywa na watumiaji wengine mfano kutuma ujumbe wa vitisho, matusi na matendo ya kihalifu. Pia usajili unasaidia kumtambulisha mtumiaji na kumwezesha kupata huduma nyingine zinazotolewa kupitia simu za mkononi mathalani huduma za kibenki, kulipa ankara na ada za shule, kutuma na kupokea pesa na huduma za intanenti.