Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

(TCRA-CCC)

Taarifa kwa Watumiaji wa Huduma za Simu

Imewekwa 25th April, 2019


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC) linawatoa hofu watumiaji wa simu za mkononi kufuatia taarifa mbalimbali zinazosambaa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu tarehe ya mwisho ya watumiaji wa simu za mkononi kuwa tarehe 1/5/2019 ni siku ya mwisho ya usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na kuwa ifikapo tarehe hiyo laini zisizosajiliwa zitafungwa kuwa taarifa hiyo sio sahihi. Kwa taarifa Zaidi bofya HAPA