Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

(TCRA-CCC)

Muundo wa Kamati za Watumiaji wa Huduma na bidhaa za mawasiliano

Wajumbe wa Kamati za Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano si wafanyakazi wa Baraza. Wajumbe ni wawakilishi kutoka katika asasi za kiraia zilizo mkoani au wilayani.

Baraza limeunda kamati za watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Lindi, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Tanga, Mbeya na Zanzibar

Lengo la Kuundwa kwa Kamati

Lengo kuu la uundwaji wa kamati za watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano ni kuhamasisha watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano nchini kuhusu haki na wajibu wao; pamoja na kukusanya maoni na kero za watumiaji na kuziwasilisha kwa Baraza.

Kazi za Kamati.

Kazi za wajumbe wa Kamati za Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano ni

  • Kuhamasisha jamii na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano juu ya haki na wajibu wao
  • Kuwasilisha taarifa zinazohusiana na sekta ya mawasiliano kutoka kwa Baraza na kuziwsilisha kwa watumiaji
  • Kukusanya maoni na kero za watumiaji na kuziwasilisha kwa Baraza.
  • Kuwasilisha kero za watumiaji na kuziwakilisha kwa watoa huduma
  • Kamati zitawasilisha ripoti za mikutano, na majadiliano yanayohusu masuala mbali mbali ya watumiaji wa huduma za mawasiliano mkoani kwa Baraza mara baada ya mikutano hiyo
  • Kamati zitaandaa ripoti ya mwaka na kuiwasilisha kwa Baraza