Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

(TCRA-CCC)

Kamati za Watumiaji

Kamati za Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano.

Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya mwaka 2003 inalipa Baraza jukumu la kuanzisha kamati za watumiaji katika ngazi ya mkoa, wilaya na sekta na kushauriana nazo.

Wajumbe wa Kamati za Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano si wafanyakazi wa Baraza. Wajumbe ni wawakilishi kutoka katika asasi za kiraia zilizo mkoani au wilayani. Baraza limeshaunda Kamati za Watumiaji katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Lindi, Mtwara, Morogoro, Mwanza, Mbeya, Tanga na Zanzibar

Lengo la Kuundwa kwa Kamati

Lengo kuu la uundwaji wa kamati za watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano ni kuhamasisha watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano nchini kuhusu haki na wajibu wao; pamoja na kukusanya maoni na kero za watumiaji na kuziwasilisha kwa Baraza.

Kazi za Kamati.

  • Kazi za wajumbe wa Kamati za Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano ni:Kuhamasisha jamii na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano juu ya haki na wajibu wao.
  • Kuwasilisha taarifa zinazohusiana na sekta ya mawasiliano kutoka kwa Baraza na kuziwsilisha kwa watumiaji
  • Kukusanya maoni na kero za watumiaji na kuziwasilisha kwa Baraza.
  • Kuwasilisha kero za watumiaji na kuziwakilisha kwa watoa huduma
  • Kamati zitawasilisha ripoti za mikutano, na majadiliano yanayohusu masuala mbali mbali ya watumiaji wa huduma za mawasiliano mkoani kw Baraza mara baada ya mikutano hiyo.
  • Kamati zitaandaa ripoti ya mwaka na kuiwasilisha kwa Baraza.